JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


VIJANA WA IRINGA WAWEZESHWA NA AIRTEL FURSA

Share This
 Mshiriki wa mafunzo ya Airtel Fursa mkoani Iringa Bi Fatuma Mkini (kushoto ) akipokea cheti cha ushiriki wa mafonzo hayo kutoka kwa afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki mara baada ya mafunzo ya Airtel Fursa kumalizika mkoani Iringa kwa vijana zaidi ya 200 kushiriki.
 Vijana washiriki wa mafunzo ya siku moja ya Airtel Fursa mkoani Iringa wakimsikiliza afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki (kulia) wakati wa ufungizi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Highland mjini Iringa jana.
Wawakilishi wa vijana zaidi ya 200 mkoani Iringa walioshiriki kupata mafunzo ya ujasiriamali kupitia mradi wa Airtel fursa wakiwa katika picha ya pamoja na afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki na wafanyakazi wengine wa Airtel mkoa wa Iringa mara baada ya kukabidhiwa  vyeti kwa niaba ya wenzao.
 (picha na mpiga picha wetu)

BAADA ya kukata tamaa ya maisha kwa muda mrefu baadhi ya vijana mkoani Iringa wameeleza kufurahishwa na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa kuwapatia mafunzo ya jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara zao kwa faida kupitia mpango wa Airtel FURSA

Wakizungumza na mara baada ya mafunzo ya siku moja ya Airtel FURSA yaliyofanyika katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa kwa kuwashirikisha vijana zaidi ya 200,washiriki hao walisema kuwa mafunzo hayo ni ukomb0zi mkubwa kwao kwani baadhi yao walikuwa wakilazimika kushinda vijiweni kutokana na kukosa fursa ya mafunzo kama hayo .

Washiriki wa mafunzo hayo Bi Husna Sanga na Bw Okelo Kasim wakizungumza kwa niaba ya wenzao walisema kuwa mbali ya kuwa wa hatua ya kampuni hiyo ya simu ya Airtel kutoa mafunzo hayo si tu kunawasaidia kupata elimu kuendesha biashara na miradi mingine ya kiuchumi bali ni sehemu ya ukombozi kwao na familia zinazowazunguka .

Alisema Bi Sanga kuwa sehemu kubwa ya vijana hasa mabinti walikuwa wakirubunika na kujiingiza katika biashara zisizofaa kama za uuzaji wa miili yao kutokana na kutokuwa na elimu ya uanzishaji wa biashara ndogo ndogo ambao zingewakomboa kiuchumi hivyo kupitia mpango huo wa Airtel FURSA ni wazi kilio chao kimepata majibu.

"Wapo baadhi ya mabinti wenzetu ambao wanalazimika kufanya biashara ya kuuza miili yao ili kupata kipato na mwisho wa siku wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa UKIMWI , ila kwa sisi ambao tumepata elimu hii kupitia Airtel FURSA tunaweza kuwa mfano kwa wengine ambao wanafikiri kazi ni kuuza miili yao pekee"

Huku Bw Kasim mbali ya kupongeza kampuni ya simu ya Airtel Tanzani kwa kuwakumbuka vijana bado alisema kuwa kama njia ya wao kupongeza kampuni hiyo ya simu kwa vijana wote waliopata mafunzo hayo kwenda kuonyesha mfano kwa wenzao kwa kufanya kazi ya kubuni miradi na kuendesha shughuli zao kifanisi zaidi.

Kwa upande wake afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki kuwa Kutokana na mradi huo wa Airtel FURSA vijana wengi watanufaika zaidi na wanafaidika na mradi huo ni wale wenye miaka kati ya 18-24

Alisema kuwa mradi huo umelenga kuwafikia vijana kote nchini na hadi sasa zaidi ya mikoa tisa wamefikiwa na mradi huo wa Airtel FURSA .

Bi Kaniki alitaja mikoa ambayo tayari imefikiwa na mradi huo Mbeya, Arusha, Dodoma, Mtwara, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam , morogoro, Tanga, Tabora na Iringa kuwa hadi sasa zaidi ya vijana 1700 wamefikiwa.

Alisema kuna njia mbili za kuwawezesha vijana njia ya kwanza kupatiwa Mafunzo ya ujasiriamali na njia ya pili kupatiwa vitendea Kazi .

Hivyo aliwataka vijana wote nchini ambao watasikia taarifa ya kuwepo kwa Airtel Fursa katika Mkoa wao basi kuweza kuchangamkia Fursa hiyo ambao hutolewa bure.

Alisema ili kijana aweze kufaidika au kushiriki kwenye Airtel FURSA atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara.

Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtelwww.airteltanzania.com

Alisema kuwa Airtel Fursa inawalenga vijana ambao wapo katika biashara na wale ambao hawana shughuli na wanataka kuanzisha shughuli pia kwao ni fursa kwao .


Aidha alisema kuwa tayari baadhi ya vijana wamepata kunufaika na mradi huo ambao umelenga kuwainua vijana na kuongeza kuwa mradi huo ulioanza mwaka huu utakuwa ni mradi endelevu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad