JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MTU MMOJA ANAYEDAIWA KUWA NI JAMBAZI SUGU ADAKWA JIJINI DAR

Share This
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, limefanikiwa kumkamata mtu mmoja anayedaiwa kuwa jambazi sugu Abdallah Said (45) kwa  makosa ya ujambazi wa kutumia silaha na uvamizi kwenye vituo vya Polisi ikiwemo kituo cha Stakishari na taasisi mbalimbali za fedha  zikiwemo benki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari , Kamishna wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa katika eneo la Kariakoo baada ya askari kufanya upelelezi wa kuwasaka watuhumiwa sugu wanaojihusisha na makosa yakiwemo ujambazi wa kutumia silaha.

Amesema  katika uchunguzi wa  wamebaini kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu kwa makosa ya  ujambazi wa kutumia silaha ikiwa ni pamoja na kufanya mauaji ya kutumia silaha.

Kamanda, Sirro amesema mtuhumiwa baada ya kufikishwa kituo cha polisi na kuhojiwa, alikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya mauaji katika kituo cha Polisi Stakishari na taasisi za fedha ambazo ni  Benki ya Access Mbagala, Benki ya NMB Mkuranga, Benki ya CRDB na CBA Chanika, Road Block ya Polisi Kongowe na matukio mengine.  

Aidha kamanda huyo  maesema kuwa mtuhumiwa huyo pia aliwataja baadhi ya viongozi waanzilishi wa mipango ya uvamizi na uporaji wa silaha na mauaji kwa kutumia pikipiki ambao ni Abdulaazizi  Ndobe, Sheykh Mtozeni, Omari Matimbwa,Haji Ulatule,Nasoro Utaule Sasoro Mpemba na wenzake.

Mtuhumiwa huyo pia alitaja mipango yote ilifanyika katika msikiti wa Kitonga na yeye akiwa mtaalam na mshauri wa kitaalam kwa upande wa utumiaji wa silaha.

Wakati huo huo.Jeshi hilo  linamtafuta, Heri Mpopezi mwenye umri kati ya miaka 35-45 kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha. Mtuhumiwa huyo ameshiriki katika matukio mbalimbali ya uvamizi wa vituo vya Polisi, na taasisi za kibenki na kupora fedha pamoja na mauaji.

Amesema mtuhumiwa huyo alikuwa mfanyakazi wa chuo  cha JKU Zanzibar na anapendelea kutembelea na kuishi Zanzibar, Chanika, Mbagala, Mbande, Kimara, Kitonga, Mwamdimkongo, Bupu, Bagamoyo,Tanga, Kilwa, Ikwiriri, Rufiji na Dondwe.

Amesema  kuwa muonekano wa mtuhumiwa huyo ni Maji ya kunde, urefu wa wastani, kipara kidogo na anapendelea kuvalia vazi la Kanzu na mavazi mengine ya kawaida. Hivyo basi, natoa rai kwa wananchi raia wema watoe taarifa za uhakika za kukamatwa  kwa mtuhumiwa huyo  kituo chochote cha Polisi.

Akizungumzia suala la Mbunge wa Singida  Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema walimkamata mbunge huyo Juni 29 mwaka huu  na wamemhoji kutokana na kutoa maneno ya uchochezi na  kutoa lugha za kashfa dhidi ya Rais Pombe Magufuli ambayo aliyatoa baada ya kutoka Mahakamani Kisutu juzi.

Tundulisu alikuwa akituhumiwa kwa kosa la uchochezi na alikuwa katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipotoka alitoa maneno ya kumkashifu Rais na maneno ya kichochezi sasa leo(jana) tumempeleka Mahakamani kujibu mashtaka hayo.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad